











Machafuko yalianzia hapa Tunisia

Baadaye machafuko yakahamia Misri

Machafuko ya Lybia
Machafuko ya Yemen

Machafuko ya Bahrain

Machafuko ya Algeria

lebanon

Morroco

Oman

Wananchi wa Syria wakizika ndugu zao katika kaburi la pamoja

Waasi wa Syria
Mateso kwa aikina mama na watoto wa Syria

Syria

Syria


Waziri mkuu wa Uingereza David
Cameroon ameitisha kikao cha dharura kwa ajili ya kujadili namna ya kutatua
mzozo wa Syria.
Majadiliano hayo yanatarajiwa
kuingilia kijeshi Syria kwa kuweka vikwazo vya anga (no fly zone) kwa serikali
ya Bwana Assad, kuwapa silaha waazi wanaipigana kuiangusha serikali ya Assad na
kuwapa moyo nchi mbalimbali kuwasaidia waasi wa Syria kwa silaha na mafunzo ya
kijeshi.
Wiki iliyopita Bwa Cameroon alitembelea
kituo kinachoongozwa na Umoja wa mataifa katika mpaka wa Syria na Jordan na
akaona mateso wanayopata maelfu ya wakimbizi kutoka Syria.
Akasema atatumaini kufanya zadi na
atafanya kazi kwa ukaribu na rais mteule wa Marekani Barack Obama katika kuzidi
kumbana Asaad ili aweze kuachia madaraka.
“Kusema ukweli kile ambacho
tumefanya hadi sasa hakijafanikiwa” alisema Bwana Cameroon
Mapema wiki hii Jenerali mkuu wa
Majeshi wa Uingereza Sir David Richards alibainisha kwamba kulikuwa na
maandalizi ya uwezekano wa kupeleka wanajeshi wa Uingereza Syria kama hali ya
kibinadamu itakuwa mbaya zaidi hasa wakati huu wa baridi kali huko Syria.
Hata hivyo alibainisha wanajeshi wa
Uingereza wanaweza kupelekwa nchi jirani na Syria ili waweze kutumika mara watakapohitajika
kama janga la kibinadamu litatokea.
Syria iliingia katika machafuko ya
maandamano ya umma yaliyoanzia Tunisia yanayojulikana kama “Arab Spring”
Maandamano hayo yamesababisha marais kama Zine El Abidine Ben Ali aliyekimbilia
uhamishoni, Hosn Mubaraka wa Misri aliyefungwa maisha, Muamar Ghadafi
aliyeuwawa kikatili. Machafuko hayo pia yalienea Yemen, Bahrain, Morocco,
Algeria na Oman
No comments:
Post a Comment