ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Thursday, December 6, 2012

Eneagram Sehemu ya Tatu. ACHIEVER


Leo ni siku ya tatu katika mtiririko wa makala yetu na kama nilivyoahidi jana, leo nitaelezea sehemu ya tatu ya aina za tabia za binadamu katika mzunguko huu  wa Eneagram. Namba tatu ni ACHIEVER/ (sikupata kiswahili chake sawia hadi sasa)
Huyu ni mtu ambaye, hufanya vizuri sana kile anachokifanya. Na hufanya kwa kuwa ni kitu kinachompa moyo. Ni mtu anayependa sana elimu. Ana maarifa mengi. Pengine ana digree zaidi ya moja au maters au PhD na tena za discipline zaidi ya moja. Utakuta anajua uingeneer, umakenika, useremala, upishi, ufugaji. Kama ni ofisini basi anajua kutengeneza komputer ikiharibika, anajua karibu kila kazi ya kitengo katika ofisi yenu. Kwake ni fahari kufanya chochote ilimradi tu anafanya vizuri na kwa mafanikio. Anaamini na kuthamini sana kile anachokifanya kwa sababu anaamini kwamba thamani yake hutokana na mambo anayofanya na nguvu yake inapatikana kutokana na shukrani na sifa anazopata kutokana na kazi zake. Mara nyingi ana shughuli nyingi kuliko muda. Muda kwake ni tatizo. Huyu ni mtu ambaye anatuliza hisia zake ili kuhakikisha kile anachofanya kinaenda kama kilivyopangwa na matokeo yake yanatoka kama yalivyotarajiwa. kwa kuwa  muda wote kuna jambo la kufanya, ni vigumu kukaa tu bila kufanya kazi. Mara zoe ukitaka appointment na mtu wa namba tatu antakuambia tu yuko busy. Huwa anakasirishwa na wageni wanaomtembelea ofisini kwake na kumkatisha kuwa "busy" anawaona kama wanampotezea muda. Yuko tayari kuchukua project ya mwenzake aifanye yeye kwa kuwa tu anayeifanya anafanya polepole mno. Namba tatu anapenda kuonekana wa kwanza katika hali yeyote ile. Namba tatu anagundulika kirahisi zaidi mashuleni au vyuoni. Yaani yeye na vitabu vitabu na yeye. Hana muda hata wa recreation. Hana muda hata wa kuongea na wengine. Ni achiever, anataka aachieve the best, na kweli ni lazima awe na max za juu kwa kuwa anaweka nguvu nyingi sana katika masomo. Akiajiriwa basi tabia ile inaendelea pia huko kazini. Utamsikia bosi akisema, "Hii kazi kama fulani hayupo haiendi kabisa" Hao ndio maachievers. Uzuri wake ni kwamba, ingawa anapenda kushindana na kuwa wa kwanza anaweza pia kushirikiana na wengine katika timu kwa kazi yeyote ilimradi tu ifanyike katika terms zake.
Udhaifu wake udanganyifu. Yuko tayari kudanganya alimradi tu afikie malengo yake " ya kuwa wa kwanza". Ukichora katika jedwali letu la enearam, utaona kwamba namba tatu anatengeneza triangle na namba sita (Doubter/hofu , mashaka) na namba tisa (Diplomat/ mambo ya watu wengine)

Endelea kufuatilia mtiririko wa makala hii ya Eneagram ili uweze kupata ufumbuzi wa namna ya kuishi na watu katika mazingira yako.
Kesho tutajadili namba nne (Romantic) hapa pana utamu sana. Usikose

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...